MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha nne

 

Sehemu ya 4: Mihadarati ya Roho

Siku iliyofuata nilianza kujisikia kama nimepata "addiction" ya halali. Yasmin alikuwa kama mihadarati ya roho  tofauti ni kwamba, badala ya kunipoteza, alinifanya nijitafute. Hakika, moyo ukishapenda kwa njia ya halali, hata shetani anakosa pa kupenya.

Saa mbili asubuhi, nilimpigia simu kwa makubaliano mapya. Nikasema, “Yasmin, nataka tuwe tunasoma pamoja Qur’an kila Jumapili.”
Akacheka, “Unatafuta njia ya kukutana na mimi kila wiki au unataka thawabu?”
Nikacheka pia, “Vyote viwili, ila thawabu ikitangulia.” 😄

Akanikubalia kwa masharti. “Ukiwahi saa nne kamili asubuhi, si saa nne na dua ya safari. Na uje na miswaki.”
Nilijiuliza, miswaki tena ya nini? Akasema, “Usisome Qur’an na mdomo wa samaki. Usinialikie azabu kwa sababu ya harufu!” 😂

Siku ya Jumapili ikafika. Nilivaa kanzu nadhifu na kubeba Qur’an yangu. Yasmin alikuja na daftari la kunukuu tafsiri. Tulikaa kwenye kivuli cha msikiti mdogo, mbali na makelele ya dunia. Tulisoma Surat An-Nur, na tulipofika aya ya 26, niliinamisha kichwa.

"Wasichana wema ni wa wavulana wema. Na wavulana wema ni wa wasichana wema..."  Qur'an 24:26

Nilimuangalia Yasmin, akasema, “Usinigeuzie macho kama mimi ni tafsiri. Angalia aya, kaka.” 😅
Nikasema, “Mwenyezi Mungu anazungumza nasi wawili hapa.”
Akacheka, “Na usome vizuri, usije ukachanganya aya ukaniambia ‘naoa Yasmin’ halafu useme ni tafsiri!”

Tuliendelea kusoma, tukachambua, tukacheka, lakini pia tulijifunza. Mapenzi ya halali ni kama kusoma Qur’an kwa pamoja hayaogopi mwanga wa mchana, wala hayaibi usiku. Yasmin alinikumbusha: “Kama unanipenda, nipe heshima na dua zako, si vocha na emojis.”