Sehemu ya 5: Kwenye Njia ya Siri
Nilikuwa nimezoea maisha ya "mapenzi ya sirini" kama WhatsApp ya usiku,Nikikesha kuchati visivyoeleweka, lakini sasa nikajikuta kwenye “mapenzi ya halali” yenye hofu ya Mwenyezi Mungu, furaha na utulivu. Yasmin alibadilisha mwelekeo wa moyo wangu kama vile Google Maps inavyogeuza safari ukienda njia mbaya. 😅
Siku moja alinipigia simu saa 11 alfajiri. “Uko tayari?”
Nikajibu, “Kwa Subhi au kwa surprise?”
Akasema, “Vyote. Leo tunaendea somo moja kwenye madrasa ya mama Fatma.”
Nikashtuka, “Na sisi ni wake wa madrasa? 😳”
Akanijibu, “Utakaa sehemu ya wanaume, mimi nitasikiliza huku na mic!”
Nilicheka, “Mbona kama unaanza kuniandaa kuwa sheikh mpenzi?” 😂
Tulifika pale madrasa. Walimu walizungumzia maadili ya ndoa kwa vijana. Yasmin alikuwa makini kama mwanafunzi anayesoma mitihani ya NECTA. Mimi nikajikuta natafakari, “Hivi mapenzi bila zinaa yana ladha gani?”
Baada ya kipindi, alinigeukia, “Sheikh wangu mtarajiwa, unadhani bado kuna future bila kupotoka?”
Nikajibu, “Ila future na wewe ni kama paradise, bora ijengwe polepole.”
Tulitembea njia fupi kuelekea kwao, lakini kwa moyo wangu, ilikuwa safari ndefu ya kujifunza kuhusu heshima. Yasmin alinikumbusha kitu cha maana sana, “Mapenzi sio tu kuhusu kukumbatiana. Bali ni kuombeana dua, kutunza nafsi yako kwa ajili ya mwingine, hata kama una nafasi ya kufanya majaribio.”
"Penzi halali halihitaji giza; linaweza kustawi hata chini ya mwangaza wa mwezi mbele ya Allah."
Kabla ya kuagana, nilitaka kumshika mkono. Akanisogea karibu na kuninong’oneza: “Ushikamane na swala kabla ya mkono wangu.” 😅
Nilibaki nimeyeyuka. Kwa mara ya kwanza, niliona mapenzi yanaweza kuwa ya nguvu bila hata kugusana.
Tulipofika nyumbani kwao, akanisalimia na kusema, “Leo umeongeza daraja, sheikh wa roho.”
Nikamjibu, “Na wewe umetupa khutba ya moyo.”
Tukacheka wote wawili... lakini roho ikabeba uzito mpya uzito wa heshima, si tamaa.