Sehemu ya 3: Chai ya mama Asia
Nilipanga tukutane tena Jumamosi asubuhi. Yasmin alipendekeza tukae sehemu tulivu yenye kahawa ya ukweli na mazungumzo ya maana. Akasema, “Sio lazima Starbucks, hata mama Ntilie anayetia baraka kwenye chai ni wa maana.”
Nikakubali bila ubishi. Mimi na chai ya maziwa? Mapenzi ya kale!
Nilifika nikiwa nimevaa kanzu ndefu na kikofia kidogo siyo kwa ajili ya show, bali kwa heshima ya siku hiyo na kumheshimu yasmin. Yasmin naye alifika akiwa kwenye hijabu ya kijani kibichi, macho yake yaking’aa kama taa za Ramadhani. Kwa kweli, moyo wangu ulichukua wudhu bila maji. 😅
Tulikaa chini ya kivuli cha mti wa mzeituni ulioko karibu na kibanda cha Mama Asia mzee mwenye tabasamu lisiloisha na mikate yenye mvuto wa dua za alfajiri. Nilitaka kuagiza chapati mbili na chai, Yasmin akanisemea: "Mimi najua wewe wa tatu hizi."
Nikamuuliza, “Unafanyaje kujua idadi ya chapati zangu?”
Akajibu kwa kucheka, “Roho ya mlo iko machoni. Na macho yako yanasema ‘chapati tatu na maziwa ya joto.’” 😄nikaona aibu kidogo.
Mazungumzo yakawa matamu kuliko chai. Yasmin aliongea kwa adabu ya hali ya juu. Hakutumia lugha ya mitaani; badala yake, kila neno lilijaa heshima, maarifa na mafundisho. Alisema, “Mapenzi si Netflix and chill… ni dua and patience. Mtu anayekupenda kweli, atajizuia kwa ajili ya kesho iliyo halali.”na si kukucheza na kukuharibia kesho yako.
"Ukiweza kumvutia kwa tabia zako kabla ya sura na miili, basi mapenzi yenu yamejengwa juu ya misingi imara si matamanio ya muda mfupi."
Tuliagana kwa staha. Hakukuwa na mikono wala vicheko vya kizembe. Aliniambia, “Ukinitaka, niombe. Na usiniandikie usiku, shetani huwa shift yake inaanza mida hiyo.”
Nikamuuliza, “Sasa nikikumiss usiku nifanyeje?”
Akajibu kwa tabasamu, “Soma Qur’an utanikuta humo, si katika DM.”