MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha tisa

🎭 Kipande 9: Siri ya Mchezo

Hoteli ya G-Luxury ilikuwa ni ya kifahari kuliko ofisi yao. Yusuph akiwa na buti zilizochakaa, koti lililochanika upande wa bega, aliingia kwa tahadhari kana kwamba anatambaa kwenye barafu nyembamba. Mapokezi, walimwangalia juu hadi chini kisha wakamuuliza: "Umealikwa kweli au umepotea njia?"

Alikuna kichwa, akatabasamu: "Nina kikao na maisha yangu." Mlinzi akamtupia macho ya mshangao, halafu akamsindikiza hadi ukumbi wa mkutano.

Alipofika, bosi mkuu alimtazama kwa jicho la ndani. "Kijana wewe ulifika kweli? Umevunja rekodi. Karibu. Kuna kitu nilitaka kukujulisha..."

Kumbe aliyepaswa kuchukua nafasi ya Yusuph aligundulika kuwa na cheti bandia! Wakati watu walikuwa wakipambana juu kwa juu, Yusuph alikuwa akipambana chini kwa chini  kwa jasho halali.

Bosi akasema: "Kuanzia leo, wewe si msaidizi tena. Umeajiriwa kama Mratibu wa Miradi Mwandamizi. Na, tuna mpango wa kukupeleka nje ya nchi kusomea uongozi zaidi!"

Ukumbi ulilipuka kwa makofi. Lakini ndani ya moyo wa Yusuph, alilia kimya kimya. Akamwambia bosi wake: "Naomba siku moja kurudi kijijini kabla ya safari, kuna mtu amenilea kwa dua."

“Aliyekusudia kutembea kwa mguu wake, hata upepo wa dhoruba haulazimishi kurudi nyuma.”    

Je, Yusuph atafika kwa mama yake kabla ya safari? Na je, kuna baraka gani zaidi zimemsubiri kijijini? Kumbuka, baadhi ya zawadi huwa hazifungwi kwa karatasi  hufunguliwa kwa machozi ya furaha!