MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha kumi

🌾 Kipande 10: Baraka Zenye Harufu ya Udongo

Yusuph alitua kijijini asubuhi ya Jumamosi. Ndege ilitua uwanja mdogo wa mkoa, kisha safari ya boda hadi kwa mama ilianza. Pamoja na mabadiliko yote aliyopitia, moyo wake ulikuwa bado ule ule  wa heshima, upole, na shukrani.

Mama yake alipotoka nje kumwona kijana wake akiwa kwenye suti, alibubujikwa na machozi. Hakusema neno hata moja. Alianguka magotini, akaelekeza uso mbinguni, na kusema: “Ewe Mola wangu, sijui majina ya baraka zako zote... lakini najua moja ya miujiza yako ni huyu hapa kijana wangu.”

Usiku ule, Yusuph aliomba mama amsamehe kwa siku zote alizoshindwa kurudi na pale ambapo aliwahi kumkosea awali. Alimkabidhi fomu ya kuandikishwa kwa safari ya Umrah. Mama hakuamini macho yake. Aliposhika fomu hiyo, alilia tena. Safari ya Yusuph haikuwa tu ya kazi ilikuwa safari ya kutimiza ndoto, na kuwaheshimu wale waliomlea kwa dua badala ya pesa.

Siku ya safari, kijiji kilikusanyika kumshuhudia mtoto wa kitongoji akiaga kwa heshima kubwa. Alizungumza machache: “Nisingekuwa mimi pasipo dua zenu. Kila jasho nililopoteza, leo limekuwa mvua ya baraka.”

“Ukiwa mti wa heri, hata ukikauka bado una mizizi ya matumaini.”        

Na hivyo ndivyo safari ya Yusuph ilivyofikia kilele  kutoka kwenye miguu iliyotembea peku, hadi kwenye ndege zilizoandikwa jina lake kama mgeni wa heshima.

Lakini daima alibeba ndani yake jina la kijiji chake, dua za mama, na jina la Mola wake. Maisha hayahitaji njia za mkato  yanahitaji subira, nia, na dua isiyokoma.

Endelea kufuatilia simulizi mbalimbali zikiwa zimebeba ujumbe na mafunzo mbalimbali.


EADRYC Boxer

©E-ONLINE

Jiunge nasi Katika group letu la Whatsapp ili kupata update za makala mbalimbali kila yanapotoka.Karibu sana!!!

Jiunge sasa