Sehemu ya 9: Kikao cha Wazazi Dakika 90 za Kuamua Hatma
Siku ilifika. Yasmin alikuwa ametulia, lakini macho yake yalionyesha msisimko wa mtu anayesubiri matokeo ya mtihani ambao hakuufanya. 😅
Tulikubaliana tukutane nyumbani kwao saa kumi jioni. Nilivaa kanzu yangu ya harusi ya mbeleni, nikaweka manukato ya "iman booster" na dua ya subira.
Nilipofika, nilikuta baba yake Yasmin ameketi sebuleni, mnyoofu kama askari wa zamani wa Jeshi la Kongo. 😬
Mama yake alikuwa na tabasamu la kutisha yaani, linacheka kwa uso lakini macho yanasema: “Unampenda binti yangu? Wewe kweli?”
Baada ya salamu, Yasmin akakaa kando ya mama yake, nami nikaketi mbele ya baba. Saa ya mahojiano ikaanza kama vile interview ya kazi serikalini.
Baba: “Kijana, unasema unampenda binti yangu?”
Mimi: “Ndio mzee, kwa heshima na kwa halal.”
Mama: “Na mapenzi yenu yamefikia wapi?”
Mimi: “Yamefikia kwenye mipaka ya dini, na malengo ya maisha.”
Baba: “Na una kazi gani?”
Mimi: “Nafanya kazi ya kujijenga ili nijenge familia.” 😅
Wote wakacheka. Yasmin akasema, “Baba, huyu siyo mchepuko. Ni kijana wa dua na bidii.”
Mama akasema, “Sasa hivi kila mtu ni ‘kijana wa dua’, lakini wengi wanatafuta ‘shortcut ya harusi ya hotelini bila baraka ya mbinguni.’”
Mazungumzo yaliendelea kwa vicheko na vizingiti, lakini mwisho wake, baba yake alisema:
“Kama kweli mnapendana, na mnaheshimiana kwa mujibu wa dini, basi mimi sina kipingamizi. Lakini mtangulizeni Mungu kabla ya mapenzi.”
Mama aliongeza, “Na kama utakula mahamri hapa, uwe na ndoa mezani siyo ahadi kwenye status ya WhatsApp.”
Tuliagana kwa furaha, huku Yasmin akinisindikiza nje kwa bashasha ya mtu aliyepata ruhusa ya kuwa halali. Aliniambia kwa sauti ya chini, “Kikao kimepita, lakini bado safari haijaisha.”
Nikajibu, “Safari hii haina shortcut, lakini ina tiketi ya peponi kama tutashikamana na uhalali.”