MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha kumi

Sehemu ya 10: Harusi Bila Filter Safari ya Halali Inapokamilika

Siku ya harusi ilipowadia, tuliamua kufanya tofauti. Yasmin alikataa makeup ya kufunika utu wake. Akasema: “Sitaki nipendwe kwa poda, nataka nipendwe kwa dua.” ❤️

Nami nilivaa kanzu na kaunda suti ya wastani, siyo tuxedo ya kigharama. Harusi ilifanyika msikitini na baada ya ndoa tukaketi kwenye uwanja wa wazi bustani ya Al-Bustan.

Baba Yasmin alifungua sherehe kwa maneno haya:

“Leo siyo mwisho wa mapenzi, bali mwanzo wa ibada ya wawili. Na ndoa hii siyo show ya Instagram, bali safari ya kujenga pepo pamoja.”

Wageni walicheka kwa bashasha, huku watoto wakikimbia na maharusi wakitoa zawadi badala ya kupokea. Yasmin na mimi tulishirikiana kuwapa keki wajane, yatima na jirani maskini.

MC alipiga utani, “Hii harusi haina dancefloor, lakini ina dua floor  ambapo mnaombewa msiachane hadi mzee mmoja aitwe ‘babu’ na mwingine ‘bibi’.” 🤣

Mzee mmoja akasema, “Hii siyo harusi ya kawaida. Hii ni ibada, na kama mtaweka Allah katikati, mtavumilia hata nyakati ambapo chumvi imeisha jikoni.”

Yasmin akanong’ona, “Hii harusi haina mbwembwe, lakini moyo wangu umejaa baraka kuliko harusi zote nilizowahi kuona kwenye TikTok.”
Nikajibu, “Tutapost picha chache  lakini tukajitahidi tupost tabia bora zaidi kwenye maisha.”

Mwisho wa siku, tukarudi nyumbani tukaswali rakaa mbili, kama waume wa kisunna na wake wa maadili. Hakukuwa na dansi wala honeymoon ya Maldives  lakini kulikuwa na baraka ya dua ya usiku wa ndoa. ❤️

Usiache kutembelea ukurasa wa simulizi Kwa simulizi mbalimbali zikiwa zimebeba ujumbe na mafunzo mbalimbali kuhusu maisha.


EADRYC Boxer

©E-ONLINE

Jiunge nasi Katika group letu la Whatsapp ili kupata update za makala mbalimbali kila yanapotoka.Karibu sana!!!

Jiunge sasa