🧱 Kipande 3: Msimamo Usio Uzika
Yusuph alianza kupata heshima kijijini. Sio kwa sababu alikuwa tajiri, bali kwa sababu hakuwahi kukwepa sala ya Subhi, hata mvua ikinyesha kama maji ya bahari. Alijulikana kama “Fundi Muislamu” na hiyo ilikuwa sifa ya dhahabu kwake ambayo alisifika nayo kijijini kwao.
Siku moja akiwa kazini, binti mmoja wa mfanyabiashara maarufu alifika kuagiza samani. Alikuwa mzuri kama mchoro wa ustadhi wa madrasa. Alimwangalia Yusuph, akatabasamu. Yusuph akainua uso, akasema: “Karibu dada yangu, karibu kwa huduma ya mbao, si ya moyo.”
Binti akacheka, “Wewe fundi bwana! Mbona una maadili kama sheikh?”
Yusuph alitabasamu tu, lakini moyoni alisema, “Si kila anayekuambia mrembo ni mchumba, wengine ni mitihani ya kujua msimamo wako.”
Usiku huo alijikuta akipambana na hisia zake mwenyewe. Alikaa kitandani na kujiuliza, “Je, nikibadili msimamo nitapata mafanikio ya haraka? Je, thamani yangu ni hadi nipoteze heshima yangu?”
“Nipo tayari kuchelewa kufanikiwa, kuliko kufika haraka kwa njia haramu.” Yusuph
Lakini kesho yake alikumbana na jaribu kubwa zaidi zawadi ya pesa nyingi ili kutengeneza samani kwa nyumba ya haramu. Yusuph aliikataa. Watu wakasema, “Huyu kijana atakufa maskini.”kutokana na kukataa ofa nono ya kutengeneza samani za haramu.
Mama yake alimwambia, “Mtoto wangu, si kila pesa ina baraka. Umetupendeza mbele ya Allah kuliko mbele ya watu.Endelea kufanya yale ambayo yatampendeza mola wako pamoja na mimi mama yako na wala usifanye yale yanayopendeza machoni mwa watu.”
🧕 Funzo: Mtu mwenye msimamo thabiti huonekana mjinga kwa muda, kisha hubadilika kuwa mfano wa kuigwa milele na kumbukumbu zake hudumu kutokana na msimamo wake.
Lakini kumbe alichokikataa kilikuwa mwanzo wa mlango mkubwa wa neema… mtu mmoja alimwona, akavutiwa naye… na akampatia nafasi isiyo ya kawaida!