🏆 Kipande 5: Mshindi Asiwe na Mipaka
Yusuph alianza rasmi mafunzo ya ujasiriamali. Alijifunza kuhusu biashara, teknolojia, hata uongozi. Wazee na vijana waliomcheka zamani walibaki wakimkodolea macho na kuanza kumuonea wivu. Hakika aliyedharauliwa sasa anaheshimika.
Lakini mafanikio yalimletea upinzani. Kwenye semina kubwa ya vijana, Yusuph alichaguliwa kuzungumza mbele ya viongozi wa serikali. Mmoja wa washiriki kijana tajiri aliyekuwa anajulikana kwa ukorofi alianza kumsema vibaya nyuma ya pazia.
“Huyu jamaa ni show-off. Eti stori ya maisha magumu? Tunaijua hiyo mbinu ya kusaka huruma…” akasema kijana huyo kwa kejeli kumkashifu yusufu.
Siku ya hotuba ilipofika, Yusuph alisimama jukwaani akiwa na kanzu nyeupe na koti la kijanja. Akasema kwa sauti yenye heshima: “Mafanikio si magari wala suti. Mafanikio ni kuwa bora kuliko jana, na kuwa na moyo safi kwa watu.”
Ukumbi mzima ulilipuka kwa makofi. Hata waliomchukia walinyamaza. Baadhi yao walitokwa machozi si kwa huzuni, bali kwa kuguswa na ukweli ambao aliuzungumza.
“Aliyepitia jua kali anaelewa thamani ya kivuli. Usimdharau mtu kwa mavazi, hujui historia ya jasho lake.” mheshimu kila unayekutana naye bila ya kujali muonekano wake.
Lakini usiku huo, alirejea chumbani kwake akiwa na barua isiyotarajiwa. Ilikuwa ni ujumbe wa hatari kutoka kwa mtu asiyejulikana: “Acha kuwa shujaa. Unaingilia maeneo yasiyokuhusu.”
Je, Yusuph atatishika na barua hii? Atasimama au atajificha? Njia ya mafanikio ya halali haijakamilika…