MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha sita

Sehemu ya 6: Siri ya Swala ya Ijumaa

Ijumaa ilifika kama kawaida, lakini haikuwa kawaida kwangu. Niliamka mapema kuliko kawaida, nilivaa kanzu safi na nikasafisha viatu kwa moyo wa mpenzi anayehudhuria harusi yake mwenyewe. 😄

Yasmin alinipigia simu akaniambia, “Leo nakutumia dua spesho. Uende masjid mapema, usome sura ya AlKahf na uombe kwa ajili yetu.”
Nikajibu, “Mbona kama najisikia kama Imam wa mahusiano?”
Akanijibu, “Imam wa moyo wangu, usiache rakaa mbili za sunnah.” 😂

Nikafika msikitini mapema sana. Niliketi mbele kabisa karibu na mimbari. Kila nikisoma Qur’an, moyo wangu ulikuwa unanong’ona jina lake. Lakini si kwa tamaa, bali kwa dua.

Baada ya khutba, Sheikh aligusia suala la vijana: “Wengi wanatafuta ndoa zenye mandhari ya sinema, lakini wanashindwa kuishi maisha ya Uislamu. Ndoa ya kweli inaanza na dua, na siyo chumbani bali msikitini.”

Nikamkumbuka Yasmin. Si kwa sababu ya sauti yake ya upole, bali kwa sababu alinivuta kwenye njia ya Mwenyezi Mungu. Mapenzi haya yalikuwa kama mto wa maziwa Jannah  hayachafuki.

Baada ya swala, nilitoka nje nikiwa na sura ya kutabasamu. Yasmin akanitumia meseji: “Umeswali vizuri, Imam wangu?”
Nikajibu: “Bado sijafika daraja lako, lakini tupo safarini.” 😄

"Mapenzi yanayoanzia kwa dua, huishi kwa rehema na hujengwa kwa heshima."

Nilitembea nyumbani kwao jioni hiyo, tukakaa nje ya mlango kama kawaida yetu. Hakuna kugusana, hakuna kuchekana sana  tulizungumza kwa staha na moyo mkunjufu.

Yasmin akaniambia, “Leo umekuwa mwanaume wa Swala.”
Nikajibu, “Na wewe ni binti wa Istiqama. Siwezi kukupoteza kwa emoji za Instagram.”
Tukacheka. Kisha tukanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa… Kimya ambacho kilijaa maneno mazito ya kimapenzi na kiroho.