MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha pili

💔 Kipande 2: Vita ya Ndani ya Kijana

Baada ya msiba wa baba yake, Yusuph alikua haraka kuliko rika lake kutokana na majukumu mazito aliyokuwa ameyabeba. Hakufahamu michezo ya PlayStation wala ladha ya chips mayai. Maisha yake yalikuwa kati ya kuchunga mbuzi na kusomea chini ya mwanga wa kibatari.

Alichokijua yeye ni Qur'an, dua, na kazi. Lakini hata hivyo, moyo wake ulitamani zaidi. Alikuwa akiona vijana wa mjini kwenye televisheni iliyokuwa ya jirani yao  akajiuliza, "Je, naweza kuwa mmoja wao bila kuuza heshima yangu?"

Siku moja aliamua kuandika barua kwa Allah! Ndiyo barua. Aliandika kwa karatasi ya daftari la zamani:

“Ewe Mola, nakuomba usinichoshe kabla sijafaulu. Nipe njia halali, siitaji shortcut. Nipe msimamo, sitaki mtego wa haraka. Ameen.”

Mama yake, kwa tabasamu la uchovu, alimwambia siku moja, “Yusuph, dunia haitoi zawadi bure, lakini Allah huwa hakosei kwa waja wake wanaovumilia.kwahiyo mwanangu wewe endelea kuvumilia Allah amekuandalia fungu lako na ninaamini siku moja utalipata katika njia zilizokuwa za halali.”

Kuanzia hapo, alianza kujifunza kazi ya useremala kwa fundi mmoja kijijini. Ingawa mishahara ilikuwa kama sadaka, lakini moyo wake ulikuwa kama milima. Hakujua siku moja somo hilo dogo lingekuwa tiketi ya mabadiliko yake...

🪵 Funzo: Hakuna kazi ndogo kwa kijana mwenye malengo makubwa. Kila jasho lina thawabu, kila uvumilivu una faida.Kamwe usiache kupambana kutokana na udogo wa kazi unayoifanya.

Lakini kilichotokea baada ya mwaka mmoja hakikuwa rahisi kuamini… ni nani aliyejitokeza ghafla kwenye maisha yake, na kugeuza kila kitu?