MYDUKA ONLINE
WhatsApp

kipande cha kwanza

 

🌧️ Kipande 1: Mwanzo wa Safari ya Machungu

Yusuph alizaliwa katika familia ya Kiislamu, kule Iringa, wilaya ya Kilolo. Wazazi wake walikuwa wakulima wa mazao ya kawaida, lakini upendo wao haukuwa wa kawaida. Walimlea kwa heshima, nidhamu na kumfundisha dini tangu akiwa na umri mdogo. Yusuph hakuwa mtoto wa starehe, bali alikuwa ni mtoto aliyeshikamana na ibada.

Mwaka 2009 ulikuwa kama radi. Baba yake, Mzee Rashid, alifariki katika ajali ya pikipiki akitoka msikitini kuelekea nyumbani. Siku hiyo ilikuwa Ijumaa  siku ambayo ilibadili kila kitu. Tangu hapo, maisha ya Yusuph yalichukua mwelekeo wa maumivu ya kila siku. Mama yake alianza kuuza karanga, na Yusuph akaanza kuchunga mbuzi. Mara nyingi alilala na tumbo tupu lakini moyo wake haukumuacha Mola wake kwa kufanya ibada na kumuomba Mola wake.

Kila usiku aliswali, akamwaga machozi kimya kimya, akisali kwa nguvu: “Ewe Mola, usiniongoze kwenye njia haramu. Nipe nguvu ya kuvuka huu mtihani.” Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa safari ngumu ya mvulana aliyekuwa na ndoto lakini hana mtaji, ana maono lakini hana msaada, ila ana MwenyeziMungu ambaye anamtegemea katika safari ya ndoto zake.

🕊️ Funzo: Hata ukizaliwa kwenye mazingira magumu, huwezi kuzaliwa bila neema. Japo dunia ina vizingiti vingi, imani ni daraja pekee linalovusha salama.

Lakini... mambo yalipoanza kuwa mabaya zaidi, ndipo miujiza ilipoanza kujitokeza. Lakini je, ilitosha? Je, Yusuph aliweza kusimama tena?